GET /api/v0.1/hansard/entries/814373/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 814373,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/814373/?format=api",
"text_counter": 334,
"type": "speech",
"speaker_name": "Lamu East, JP",
"speaker_title": "Hon. Ali Sharif",
"speaker": {
"id": 2100,
"legal_name": "Shariff Athman Ali",
"slug": "shariff-athman-ali"
},
"content": " Asante, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Ningependa kuungana na wenzangu kuunga mkono Mswada huu ambao uko mbele yetu hapa leo. Nikiamini pakubwa, ni Mswada ambao wakenya wamekuwa wakiusubiri kwa siku nyingi sana. Hakukua na mwongozo kamili katika swala hili nzima ya maswala ya ardhi. Ingawaje mwaka wa 2010 Wakenya walipitisha Katiba, miongoni mwao yalikua ni haya ya kuweka Tume ya Ardhi ili kusawazisha tatizo hili la ardhi. Leo hii tutapata kwamba, Kenya nzima, sana sana Pwani ambako nimetoka kumekua na tatizo kubwa katika swala la ardhi. Matatizo haya yamesababishwa na kutokuwa na mwongozo kamili katika swala hili, kwa namna watu wanafidiwa wakati wanapopokonywa sehemu zao ama ardhi zao zinachukuliwa na Serikali. Naona Mswada huu umeangazia mambo muhimu sana. Miongoni mwao ni utaratibu ambao namna wale ambao wameweza kuchukuliwa ardhi zao watakavyolipwa pesa zao na namna Serikali itakavyochukua utaratibu huu. Huu ni utaratibu ambao uko sawa isipokuwa, unahitaji kutiliwa mkazo katika maadili ama utekelezaji wa swala hili kwa ujumla. Tayari tumeona katika Kaunti ya Lamu tuna matatizo haya mpaka sasa tunavyozungumza, watu wameweza kusikiliza amri ya Serikali na kutoa ardhi zao. Mpaka sasa tunavyozungumza, watu hawa wameathirika kwa muda wa takriban miaka mitano hivi sasa na hakujakuwa na mwongozo wowote kwa Serikali namna ya kufidia watu hawa. Kutokana na hayo, ndiposa nikasema kuwa naamini kuwa ni Mswada ambao utakuwa na mwongozo katika swala hili. Vile vile, jopo ambalo naona hapa litaundwa kutembea na kusikiliza malalamishi kama haya ni jopo muhimu sana. Naliunga mkono kwa sababu matatizo mengi yemekuwepo. Naamini pakubwa ili Serikali ijiendeleza na miradi yake, bado inahitaji ardhi nyingi ambazo hivi sasa zinamilikiwa na watu binafsi ama mashirika. Kutokana na hayo, ili nchi hii iweze kujimudu na kujiendeleza kiuchumi ni lazima ardhi hizi ziwe na utaratibu wa kupatiwa kwa Serikali kwa sababu miradi hii ina mipangilio ya kiserikali. Miongoni mwa mambo ambayo tunayaona wazi ni barabara zetu ambazo zinahitaji kupanuliwa. Hali halisi ya nchi yetu ni kwamba barabara zetu vile zilivyo zahitaji kupanuliwa. Kutokana na hiyo, itabidi Serikali itumie mbinu hizi ambazo twazungumzia leo za kuchukua ardhi hizi kwa utaratibu huu, na wale wenye sehemu hizi ambazo watapeana kwa Serikali kwa sababu ya mambo kama haya na kurahisisha usafiri ni kwamba utaratibu huu utakapofanyika kwa njia zake, sidhani kama kutakuwa na tatizo lolote. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}