GET /api/v0.1/hansard/entries/814374/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 814374,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/814374/?format=api",
"text_counter": 335,
"type": "speech",
"speaker_name": "Lamu East, JP",
"speaker_title": "Hon. Ali Sharif",
"speaker": {
"id": 2100,
"legal_name": "Shariff Athman Ali",
"slug": "shariff-athman-ali"
},
"content": "Ningependa kuunga mkono wenzangu na ningeomba Serikali ihakikishe kwamba utaratibu huu umefuatwa kikamilifu na wale wote ambao wataathirika na swala hili wazingatiwe kikamilifu na kupewa haki zao. Ili amani kupatikana na mwongozo ama uchumi kuendelea kisawasawa katika nchi hii, ni lazima haki ya kila Mkenya ipatikane. Kama nilivyosema, ni tatizo ambalo limekuwa kwa siku nyingi sana, hasa katika sehemu ya Pwani. Tumeona mara kwa mara watu wamepokonywa sehemu zao na Serikali kwa njia za mabavu ama za kulazimishwa na hakuna lolote ambalo linafidiwa. Hufika wakati mtu anapokonywa haki yake akiwa ameshika hati miliki mkononi. Haya tumeyashuhudia na ni mambo ambayo hayapendezi katika nchi hii. Naamini pakubwa kutokana na Mswada huu ni mambo ambayo tutaweza kusawazisha. Vile vile, ningependa kuzungumzia swala hili la namna watu watakavyofidiwa. Ikiwa Mswada huu utabakisha kusema kwamba fidia hii itakuwa ni maswala ya pesa, ardhi na kadhalika lakini iwekwe kipengele kinachosema kwamba haya yatapatikana kwa ushauriano na yule atakayeathirika, itakuwa vizuri. Libaki swala la pesa peke yake ama ikiwa yatabaki maswala haya mengine kama ardhi nyingine ama bondi, kuwe na kipengele kinachosema kuwa haya yatapatikana kutokana na uwiano baina ya Serikali, tribunal ama kamisheni na kusema ya kwamba yule atakayeathirika kile atakachochagua katika hizi mbinu ambazo ziko hapa, isiwe ni lazima. Kwa hivyo, kuwe na sehemu ambayo itaonyesha kwamba ili kupatikana haya ama kufanyika hili, lazima kuwe na uwiano baina ya yule aliyeathirika na Serikali kuhusiana na maswala haya ya fidia. Vile vile, utaratibu ambao utatumika…"
}