GET /api/v0.1/hansard/entries/814382/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 814382,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/814382/?format=api",
"text_counter": 343,
"type": "speech",
"speaker_name": "Cherangany, JP",
"speaker_title": "Hon. Joshua Kutuny",
"speaker": {
"id": 61,
"legal_name": "Joshua Serem Kutuny",
"slug": "joshua-kutuny"
},
"content": " Asante, Mhe Naibu Spika wa Muda. Kwa sehemu ambayo amesema kwamba yule ambaye anatakikana kufidiwa atashurutishwa, ukisoma kwenye Mswada huu ambao tumeutengeneza kama kamati, hakuna mtu ambaye atashurutishwa jinsi ya kufidiwa. Itakuwa yeye mwenyewe kuchagua jinsi atakavyofidiwa. Kama hatataka malimbikizi kutoka kwa Serikali, itakuwa sawa. Kama hataki ardhi mbadala, itakuwa sawa. Kama anataka hundi kutoka kwa Serikali, ni sawa. Kwa hivyo, itakuwa muhimu kwa Mheshimiwa kuelewa kwamba, hakuna mtu atashurutishwa. Itakuwa kwa hiyari jinsi ya kufidiwa. Asante."
}