GET /api/v0.1/hansard/entries/814385/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 814385,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/814385/?format=api",
    "text_counter": 346,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu East, JP",
    "speaker_title": "Hon. Ali Sharif",
    "speaker": {
        "id": 2100,
        "legal_name": "Shariff Athman Ali",
        "slug": "shariff-athman-ali"
    },
    "content": "mtu atalazimika, lakini Mswada haujawekwa wazi. Hofu yangu ni kwamba kumewekwa utaratibu wa kusema kwamba ni maswala ya pesa, ardhi, bondi na kadhalika. Moja ya hizi. Ningeomba kwamba, katika hizi kuwe na kufahamika kwamba kutakuwa na maridhiano. Ndilo neno ambalo nataka liwepo hapa, kwa sababu tunapowacha wazi ni kuonyesha kwamba ni mtu atachagua mwenyewe. Lakini inafika wakati kulingana na hali tunavyoiona, wale wahusika wakuu wenye mamlaka au majukumu ya kuendesha haya inafika wakati wanakwenda na maamuzi yale wanayotaka wao. Haya tumeyaona yakifanyika katika nchi yetu. Mtu anakwenda na maamuzi, anasema ni hivi, ilhali kuna namna nyingine ya kusuluhisha swala lile. Hiyo ndiyo hofu yangu. Kwa hayo ambayo nimeweza kuchangia, naunga mkono Mswada huu na nawapongeza wale wote ambao walikaa kulifikiria swala hili na kuileta hapa kwa wakati mwafaka kama huu, huku tukiamini pakubwa kama viongozi Wakenya wanaendelea kuteseka kwa matatizo haya ambayo tunayajadili leo. Asante Mhe. Naibu Spika wa Muda."
}