GET /api/v0.1/hansard/entries/814566/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 814566,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/814566/?format=api",
"text_counter": 173,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "tunaongozwa na Katiba moja. Kwa hivyo, lazima tuisome hiyo Katiba na tujue majukumu yetu kama Wabunge na Maseneta katika Jamhuri ya Kenya. Mheshimiwa Naibu Spika, hili suala la sheria tunazopitisha hapa kwenda katika Bunge la Kitaifa na kudharauliwa sio katika majukumu ya sheria peke yake. Hata zile kanuni tunazoangalia katika Kamati yetu ya “Delegated Legislation” pia zinapoenda kule, nyingi hutupwa nje kwa sababu ndogo ndogo zisizo halisi. Kwa hivyo, wakati umefika kwa ofisi yako – kama kiongozi wa Bunge hili, na ofisi ya Spika wa Bunge la Kitaifa – mkae chini ili mtatue mizozo hii inayoibuka mara kwa mara. Hii ni kwa sababu sio katika maadili ya kitaifa kwamba bunge mbili zinateta mara kwa mara. Mheshimiwa Naibu Spika, Bunge la Seneti ni Bunge la waungwana, wazee na watu wenye busara nyingi. Kwa hivyo, hailingani na maadili ya kitaifa kuwa tunalumbana mara kwa mara na watu ambao hawajajua majukumu yao kikamilifu. Iwapo utatumia fursa hii na ofisi yako kuleta uwiano baina ya bunge zote mbili, itakuwa ni jambo kubwa la kusaidia taifa letu kusonga mbele. Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la Constituency Development Fund (CDF) limezungumzwa hapa. Utaskia kwamba shule za chekechea zinajengwa na kaunti, halafu CDF inajenga shule za msingi na za upili. Jambo hili sio sawa kwa sababu shule za chekechea zinajengwa vizuri, halafu Wabunge wanakuja na kuzikabidhi kwa serikali ya Kitaifa bila sisi, Maseneta kujua. Kwa hivyo, majukumu mengi yanayofanyika---"
}