GET /api/v0.1/hansard/entries/814582/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 814582,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/814582/?format=api",
    "text_counter": 189,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Boy",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13200,
        "legal_name": "Issa Juma Boy",
        "slug": "issa-juma-boy"
    },
    "content": "Asante sana, Bw. Naibu Spika. Nitachukua muda mfupi sana. Kwanza, ninataka kuunga mkono jambo liloletwa hapa na kiongozi wa wengi; Sen. Murkomen. Kama unavyojua, sisi Maseneta ni watu muhimu sana katika nchi hii, hasa katika kaunti. Hakuna mtu ambaye anaangalia rasilmali ya kaunti na kila kitu katika kaunti isipokuwa Bunge la Seneti. Hawa Wabunge wenzetu katika Bunge la Kitaifa wanafikiria ya kwamba sisi Maseneta tutaacha useneta na kwenda katika ugavana miaka inayokuja. Hii ndiyo shida yao kubwa. Mimi ningeomba Seneta wenzangu tuungane ili tuweze kupigania Bunge letu la Seneti na kuhakikisha kwamba Seneti inaheshimiwa na isimame imara kuwatumikia wananchi wetu katika nchini na kaunti zetu. Ndugu zangu Maseneta, tunapigwa vita na wenzetu katika Bunge la Kitaifa. Tungeomba Spika wa Seneti na yule wa Bunge la Kitaifa waketi pamoja ili kuhakikisha kwamba Bunge zote mbili zinaheshimiana. Kwa hayo machache, ninaunga mkono."
}