GET /api/v0.1/hansard/entries/816709/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 816709,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/816709/?format=api",
    "text_counter": 232,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu CWR, JP",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Ruweida Obo",
    "speaker": {
        "id": 786,
        "legal_name": "Ruweida Mohamed Obo",
        "slug": "ruweida-mohamed-obo"
    },
    "content": " Ahsante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi name nichangie Hoja hii inaopendekeza kuwekwa kwa kamera katika shule za upili. Naona kuweka kamera hizo ni jambo la muhimu sana. Zitasaidia sana kuzuia uhalifu tofauti tofauti katika shule.Itasaidia kaunti pia. Kwa mfano, itasaidia Lamu katika wadi ya Basuba. Najua hata wakiniona nachangia mambo ya kamera, wanashangaa sana. Wadi ya Basuba haina hata shule moja ya upili. Mtu akizungumzia mambo ya kamera, nashangaa sana kwa sababu kule Basuba hatuna hata walimu katika shule za msingi. Shule tano zimefungwa. Wanafunzi wanaenda kusoma huko Hindiwood. Nasisitiza kuwa kamati ya elimu iliangalie suala hili zaidi. Inasikitisha kwamba watu wanazungumzia mambo ya kwenda mbele ilhali wengine wanazungumzia kamera na mambo mengine. Mahali kama Kiangwi, Milimani, Basuba na kwingineko, shule zote zimefungwa na hatujui walimu watarudishwa lini. Ni lazima waangalie suala hili kwa kina. Tunaambia Wakenya eti ni sawa lakini bado hatujajua ni sawa kivipi. Bado watu wa wadi ya Basuba wanaona haijakuwa sawa."
}