GET /api/v0.1/hansard/entries/816753/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 816753,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/816753/?format=api",
    "text_counter": 276,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kilifi CWR, ODM",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Gertrude Mwanyanje",
    "speaker": {
        "id": 13245,
        "legal_name": "Gertrude Mbeyu Mwanyanje",
        "slug": "gertrude-mbeyu-mwanyanje"
    },
    "content": " Ahsante sana, Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda. Ninachukuwa fursa hii kumuunga mkono Mbunge wangu Mheshimiwa Owen wa Kilifi Kaskazini kwa kuleta Hoja hii hapa. Mkorosho na korosho zake umekuwa mmea muhimu sana katika jimbo la Pwani na hasa katika Kaunti ya Kilifi. Tuko hapa kuunga mkono kurejeshwa upya na kuanzishwa tena kampuni ya Mkorosho pale Kilifi. Kwa wakati huu tunaiomba Serikali iweze kutia maanani kuwa mkorosho ni kati ya mimea ile muhimu sana katika biashara zote ikilinganishwa na kahawa na chai ambazo zinakuzwa kule nyanda za juu."
}