GET /api/v0.1/hansard/entries/816754/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 816754,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/816754/?format=api",
"text_counter": 277,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kilifi CWR, ODM",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Gertrude Mwanyanje",
"speaker": {
"id": 13245,
"legal_name": "Gertrude Mbeyu Mwanyanje",
"slug": "gertrude-mbeyu-mwanyanje"
},
"content": "Kampuni ya mkorosho ilikuwa imepebuni kazi nyingi katika miaka ya tisini hasa kwa akina mama. Palikuwa na akina mama zaidi ya mia sita ndani ya kampuni hiyo. Kiwanda hiki kilipofilisika, familia nyingi zilisambaratika. Wengi wetu katika jimbo la Kilifi tumesoma kwa sababu ya pesa ya korosho. Wamama walijitegemea ndani ya jimbo la Kilifi; hawakungoja baba aje nyumbani ndiposa waweze kuwa na chakula. Pia, hawakungoja watoto watoke kazini ndipo waweke chakula juu ya meza. Kufilisika kwa mkorosho huu kumeleta shida ya makaazi ndani ya jimbo la KiIifi na eneo la Pwani lote."
}