GET /api/v0.1/hansard/entries/816755/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 816755,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/816755/?format=api",
"text_counter": 278,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kilifi CWR, ODM",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Gertrude Mwanyanje",
"speaker": {
"id": 13245,
"legal_name": "Gertrude Mbeyu Mwanyanje",
"slug": "gertrude-mbeyu-mwanyanje"
},
"content": "Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda, sababu mojawapo ya kuwa na vijana ambao wanazurura ovyo ni kukosa hata mtambo mmoja katika jimbo la Kilifi. Lakini kurejeshwa kwa mtambo huu, kutabuni kazi kwa vijana, akina mama na akina baba. Kwa sababu wakati huu tutaanza upya kupanda mikorosho, ni ombi langu kwa wakaaji wa Kilifi kwamba waweze kupeana mashamba yao makubwa ambayo yamekaa bila kutumika ili tuweze kupanda kwa wingi. Mkorosho huu ulianzishwa upya upandaji pale Kilifi mwezi uliopita na tuko na marafiki ambao wako tayari kutuunga mkono kuupanda. Tuweze kuona ni vipi Serikali itaweza kuweka pesa zaidi ya upandaji wa mikorosho ndani ya kaunti ya Kilifi. Tukifanya hivyo, tuone vipi bidhaa ya korosho itawezesha kurejeshwa kwa mtambo huu hasa katika wadi ya Kibarani ambapo mimi nilikuwa mwakilishi mnamo 2013. Sehemu nyingine ya kuangaliwa ni Ganze. Sharti tuone ni vipi mtambo huu na bidhaa zake zaweza kufufua maisha ya biashara kwa wakaazi wa Kilifi. Ahsante."
}