GET /api/v0.1/hansard/entries/816758/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 816758,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/816758/?format=api",
    "text_counter": 281,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Magarini, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Michael Kingi",
    "speaker": {
        "id": 13412,
        "legal_name": "Michael Thoyah Kingi",
        "slug": "michael-thoyah-kingi"
    },
    "content": "Kwanza, tunavyojua, mkorosho ukilinganishwa na mimea mingine ambayo imepandwa katika sehemu nyingine za nchi kama vile kahawa ama majani chai utaona kwamba mkorosho ni rahisi sana kukuza. Ile mbolea ambayo inatakikana ili kukuza kahawa au majani chai si ile ambayo inahitajika kukuza mkorosho. Kwa hivyo, kukuza mkorosho huwa ni rahisi zaidi. Hii ndio imefanya mkaazi wa Kilifi kuhakikisha kwamba anautunza kwa vile unaleta mazao kwa urahisi. Mkorosho umekuwa ukichangia sana maisha mema kwa wakazi wa Kilifi na Pwani. Saa hii, kwa sababu kiwanda hiki cha korosho ama sekta hii ya korosho imefifia ndani ya Kilifi na Pwani, wananchi wengi wanauza ardhi zao. Hii imechangia umaskini katika sehemu zile. Kitambo sisi tukisoma, ilikuwa rahisi. Unaingia shambani, unaokota korosho, unaenda kuuza na unanunua kitabu na kalamu bila hata kumsumbua mzazi lakini tangu sekta hii ya kukuza korosho ififie, hali ya maisha imekuwa ngumu. Kama tumeongea kwamba Kenya hii ni lazima kuwe na viwanda ili tulete ajira kwa watu wetu, ni lazima sekta hii ya korosho ifufuliwe. Ninajua sekta hii ikifufuliwa vijana na kina mama wa Pwani na Kenya kwa jumla watapata kazi kwa sababu kutakuwa na wakulima, wanaokota korosho na wanaouza korosho. Kutakuwa na kazi tofauti. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}