GET /api/v0.1/hansard/entries/816759/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 816759,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/816759/?format=api",
"text_counter": 282,
"type": "speech",
"speaker_name": "Magarini, ODM",
"speaker_title": "Hon. Michael Kingi",
"speaker": {
"id": 13412,
"legal_name": "Michael Thoyah Kingi",
"slug": "michael-thoyah-kingi"
},
"content": "Mapato ya mkorosho yatachangia sana. Mkazi wa Kilifi na Pwani kwa jumla ataweza kuweka chakula juu ya meza. Tutahakikisha kuwa hakuna wakati hata mmoja tutahangaika na kuomba serikali kwamba tunataka chakula cha msaada. Hii ni kwa sababu njaa inapokuwa nchini utaona ni Ganze, Kilifi ama Magarini. Ni kwa sababu serikali haijawawezesha wakaazi wa Pwani, Kilifi, Magarini au Ganze, sehemu ambazo ni rahisi kabisa ambazo tukizifufua tutahakikisha kwamba wakazi wanapata mapato ya ziada."
}