GET /api/v0.1/hansard/entries/816763/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 816763,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/816763/?format=api",
    "text_counter": 286,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Jomvu, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Bady Twalib",
    "speaker": {
        "id": 1612,
        "legal_name": "Bady Twalib Bady",
        "slug": "bady-twalib-bady"
    },
    "content": " Asante, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia fursa hii leo ili niunge mkono Hoja hii ambayo imeletwa na ndugu yetu Owen Baya ambaye ni Mbunge kutoka Kilifi kuhusu mambo ya mkorosho. Kusema kweli, jambo hili ni la maana sana kwa sisi Wapwani kwa sababu ni muda mrefu sana ambapo Pwani ilibobea kwa mambo ya ukulima, na hasa ukulima wa korosho mpaka tukaona katika sehemu ya kilifi kulikuwa na mtambo mkubwa sana wa kusaga korosho. Mpaka dakika hii mtambo ule umekufa. Itakumbukwa vizuri kabisa kuwa mleta Hoja hii ametoa mifano kadha wa kadha. Ni dhahiri wengi tunaosafiri kwa ndege tunapewa korosho na tukiuliza korosho zile ambazo tunapewa ndani ya ndege zinatoka wapi twasikia, “korosho hizi zimeletwa kutoka nchi nyingine.” Mimi ninashangaa kwa sababu tukiangalia pale Pwani, korosho zilikuwa nyingi lakini tukipaa kwenye ndege tunapewa korosho kutoka kwingine, ilhali kwetu korosho zile zaweza kumea. Hili ni jambo la kutamausha sana. Hii ndio maana kwenye Bunge hili, siku zote kuna msemo mimi hupenda kuutumia kuwa mambo haya ya kuturudisha nyuma ni kama ule msemo wa goji kirba kirba goji, yani badala ya kutupeleka mbele, wanaturegesha nyuma. Nchi ya Tanzania hivi sasa imebobea katika mambo ya ukuzaji wa korosho. Kuna Bandari za Dar es Salaam na Tanga lakini ukifika katika Bandari ya Bagamoyo katika Tanzania, biashara nyingi ambayo inafanyiwa kazi hapo ni biashara ya kusafirisha korosho. Sisi ndani ya Kilifi na Pwani nzima kwa jumla tungependa kuona Hoja hii imetiliwa mkazo na vile vile ukuzaji wa korosho uweze kuendelea. Ninasema hivyo kwa sababu katika Ajenda kuu za Serikali hii tuliyo nayo, moja ni mambo ya nyumba, nyingine ni matibabu bora, nyingine ni mambo ya chakula ambayo ni food security na vile vile industrialisation, ambayo ni mambo ya viwanda. Katika kuitimiza moja ya Ajenda ya Serikali hii, ni muhimu tufufue viwanda. Katika kufufua viwanda, moja kati ya viwanda hivyo kiwe ni hiki kiwanda cha korosho kulingana na Hoja hii ambayo imeletwa. Lakini isiwe tu ni kiwanda cha korosho kinachofufuliwa. Kuna viwanda tofauti tofauti kama vile kiwanda cha Associated Vehicle Assemblers (AVA) cha kutengeneza magari ambacho kiko kwangu na vile vile kiwanda kikubwa cha kutengenza chuma cha Kenya United Steel Company (KUSCO). Vile vile kuna kiwanda cha Kenya Meat Commission (KMC). Viwanda hivi tukiweza kuvifungua katika Ajenda ya Serikali, basi bila shaka tutaweza kuwaajiri vijana wengi. Vijana ambao tumewaajiri watapata kuenda shule na vile vile wazazi wetu ambao watakuwa wakifanya kazi katika sehemu hiyo wataweza kufaidika. Kwa hivyo, leo hii ni fursa kubwa sana ambayo tumeipata sisi Wabunge kutoka Pwani kuiunga mkono Hoja hii ambayo imeletwa na ndugu yetu, Mheshimiwa Owen Baya. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}