GET /api/v0.1/hansard/entries/816768/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 816768,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/816768/?format=api",
"text_counter": 291,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante sana Mheshimiwa Spika, ama kweli Kiswahili kitukuzwe. Ninachukua nafasi hii kwanza kumpongeza sana Mheshimiwa Owen ambaye ameileta Hoja hii. Ukulima wa korosho na mkorosho kwa jumla ni mmea wa kitaifa. Kwa sababu hiyo, upandaji wa mmea huu wa korosho na mazao yake, hasa yanapatikana katika ukanda wa Pwani. Mhe. Spika wa Muda, ninataka niseme kwamba kiwanda cha korosho kilichokuwa na sifa mwaka wa 1974 hadi mwaka wa 1992, kilikuwa kinaitwa “Kenya Cashew Nuts”. Kilikuwa maeneo ya Kaunti ya kilifi. Ninataka nichukue nafasi hii kwanza niwajuze kwamba kauli ya Rais wa Jamhuri yetu ya Kenya, Mhe. Uhuru Muigai Kenyatta, Mhe. William Samoei Ruto, Chama cha Jubilee kwa jumla na sisi ambao tuko ndani ya Chama hicho hivi sasa, ni kwamba kuna Agenda Nne Kuu. Moja yapo katika zile Agenda Kuu Nne ambazo Mhe. Rais amezipigia mbiu sana ni uboreshaji na ubunifu wa viwanda katika Jamhuri yetu ya Kenya. Ni jambo ambalo analitilia mkazo sana. Ninataka kuliunga mkono kwa dhati nikiwa na tamaa yote kama mkaazi wa kutoka Pwani, Kaunti ya Kilifi na Mkenya kwa jumla. Kiwanda hiki cha korosho ambacho tumekikosa kwa muda kilikuwa kikileta manufaa mengi ya kiuchumi katika maeneo ya ukanda wa Pwani na taifa nzima, kitapewa kipaumbele na kitaanzishwa upya. Kwanza, kitabuni nafasi za kazi na vile vile kuleta mapato katika kapu la kitaifa ambalo ni mapato yetu katika taifa nzima. Zamani tulikuwa tunaona kwamba linachangiwa kabisa. Asilimia nne ya mapato katika mradi mzima wa korosho ama viwanda vyote vitano vilikuwa vimeboreshwa katika taifa letu la Kenya."
}