GET /api/v0.1/hansard/entries/816777/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 816777,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/816777/?format=api",
"text_counter": 300,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kinango, ODM",
"speaker_title": "Hon. Benjamin Tayari",
"speaker": {
"id": 13379,
"legal_name": "Benjamin Dalu Stephen Tayari",
"slug": "benjamin-dalu-stephen-tayari-2"
},
"content": " Ahsante sana, Mhe. Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii ili nichangie Hoja hii kuhusu suala la kurejesha mtambo wa korosho katika eneo la Pwani. Kwanza kabisa ninamshukuru Mhe. Baya kwa kutuwakilisha vizuri kwa kuleta Hoja hii ambayo inatuhusu sana sisi wakaaji wa Pwani. Kusema kweli, korosho ni mmea ambao umesaidia sana watu wa Pwani. Mimi nikiwa mmoja wao, ninaelewa kwamba kule ukanda wa kutoka Kwale kwenda mpaka Kilifi tumelelewa na zao la korosho. Tukiwa wadogo, tulikuwa tunachukua korosho, tunaipeleka kupima, inapelekwa mtamboni na inatusaidia kulipa karo na mambo mengine. Lakini hivi sasa bei ya korosho imeshuka mpaka Kshs20 kwa kilo kwa zile ambazo hazijatayarishwa. Ukiangalia dunia nzima, kilo moja ya korosho ni Kshs200. Kwa hivyo, kama Wakenya, ni lazima tulitilie maanani hili suala la korosho na tuhakikishe kwamba tunaangalia korosho kama mimea mingine kama majani chai na kahawa. Hiyo itatusaidia sana kwa sababu itaongeza kitu katika kikapu cha uchumi wa nchi hii. Kuongezea haya, ni lazima pia tuangalie kwamba tunapatia wakulima wa Pwani mbegu nzuri ambazo zinaongeza usalishaji wa korosho. Hivi sasa, mikorosho ambayo iko huko ni ya samani na imezeeka. Lazima Serikali ipeane mbegu ya kisasa. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}