GET /api/v0.1/hansard/entries/817862/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 817862,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/817862/?format=api",
    "text_counter": 442,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Mashariki inaathiri sehemu za Lamu na Tana River ambako kuna wizi wa ng’ombe na maghaidi wa Al Shaabab ambao wanavamia sehemu za Lamu na kwingineko. Tatizo la Kaskazini Mashariki si la sasa. Ni tatizo ambalo limekuwa kwa muda mrefu. Kulikuwa na upungufu wa waalimu, madarasa na shule ambazo ziko kule bado hazijaboreshwa. Katika sehemu zingine wanafunzi wanaingia shule kupitia vitambulisho vya biometric vya kisasa. Shule nyingi mjini Nairobi zimeanzisha mfumo huo, lakini kule Kaskazini Mashariki hata madarasa hayapo katika shule nyingi. Katika shule nyingi wanafunzi wanakaa chini ya miti. Kwa hivyo, walimu wanaosomesha sehemu zile hawana motisha ya kufunza vizuri. Bi.Spika wa Muda, tatizo kuu ni maendeleo. Ili kuwe na maendeleo ni lazima tuwe na shule nzuri, mabweni na madarasa ya kisasa. Walimu watakuwa na hamu na ari ya kwenda kufundisha katika sehemu kama zile. Lakini ikiwa maendeleo yatakuwa bado ni duni katika sehemu zile, walimu wengi hawatakuwa na hamu ya kufanya kazi katika sehemu kama zile. Hakuna mtu anayetaka kufanya kazi katika sehemu ambazo hazina maendeleo na malazi na vyoo sawa au maji ya mfereji. Vile vile hakuna mtu anayetaka kufanya kazi katika sehemu ambayo haina umeme katika shule na makaazi watakaoishi. Kwa hivyo, ni lazima maendeleo yafanyike katika sehemu zile. Lazima Serikali ijenge shule za kisasa na iendeleze sehemu zile kwa kupeleka maji, umeme na idumishe usalama. Hii ni kwa sababu usalama unahakikishia kila mtu kwamba ana haki ya kuishi na kufanya kazi katika sehemu yeyote ambayo anapendezwa. Jambo la pili ni kwamba ni lazima tuangalie hali ya utamaduni ya zile sehemu. Kwa mfano, watu wengi kutoka sehemu zile zinazozungumziwa ni Waislamu na wanajaribu kulinda utamaduni wao wa Kiislamu. Kwa hivyo, hatuwezi kusema kwamba walimu wote watakaopelekwa kule watakuwa, kwa mfano, wa dini tofauti na ya Kiislamu. Ni lazima tuhakikishe kwamba katika sehemu kama zile tunapata walimu wengi ambao wanatoka katika makabila yao ama tamaduni ambazo zinaingiliana. Kwa mfano, walimu ambao ni Waislamu watajumuika kwa urahisi na wakaazi wengine wa Kaskazini Mashariki kuliko walimu wa imani ingine. Bi. Spika wa Muda, kwa hivyo, ni lazima tuangalie huu utamaduni kwa makini. Ninahakika ya kwamba, wanafunzi wengi ambao labda hawafanyi vizuri katika elimu ya darasani kule North Eastern, wanafanya vizuri katika elimu ya dini. Hiyo inamaanisha kwamba, walimu wanaosomesha dini wanaweza kupewa fursa ya kuenda katika vyuo vya ualimu na wapewe somo la Kiingereza peke yake ili wahakikishe ya kwamba wanaweza somesha kwa Kiswahili, Kiingereza na Kiarabu. Kwa hivyo, wakati mwanafunzi yuko darasani katika sehemu zile za North"
}