GET /api/v0.1/hansard/entries/817930/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 817930,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/817930/?format=api",
    "text_counter": 44,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mwatate, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Andrew Mwadime",
    "speaker": {
        "id": 2451,
        "legal_name": "Andrew Mwadime",
        "slug": "andrew-mwadime"
    },
    "content": " Asante, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kuingilia kati kupunguza hizo kelele za wenzangu. Kabla sijaanza kuendelea kuongea, ningependa kusifu Bunge kwa kutuletea aina ya tarakilishi hapa ingawa tungependa waiboreshe zaidi iwe na mambo mengi; Hoja zote ziwe ndani ya hii tarakilishi. Wale walikuwa miaka ya themanini, wakati kile kiwanda kilikuwa kinafanya kazi, watu wengi sana walikuwa wameajiriwa na kile kiwanda. Si watu wa Kilifi pekee. Ilikuwa ni Wakenya wengi kwa ujumla. Watu wa Lamu, Tana River, Kwale, Taita Taveta, Mombasa na Wakenya wengine kote nchini walikuwa wameandikwa. Walikuwa wengi. Vile vile, akina mama walikuwa na shughuli kule mashinani maanake walikuwa wanashughulikia hizi korosho. Akina baba walikuwa wanashughulikia hizi korosho. Masuala ya mihadarati yalikuwa kidogo wakati ule maanake watu walikuwa na shughuli wanafanya. Baada ya kiwanda kuvunjika, mambo yamekuwa mabaya sana kule Kilifi. Kilimo cha korosho ilikuwa shughuli zaidi kule Kilifi. Mapato yao mengi yalikuwa yanatokea kwa korosho. Ni vyema Serikali itambue kwamba kazi na lishe kwa watu wa Kilifi ilitoka hapo. Hata mapato makubwa yalikuwa yanatokea hapo. Kufufua hiki kiwanda kutasaidia nchi kwa ukubwa maana vijana watapata kazi, lishe kwa wenyeji wa pale itakuwa sawa na nchi itapata ushuru mkubwa. Nashangaa juzi nilipochukua ndege kutoka Nairobi kwenda Mombasa, niliona korosho katika kipaketi. Nilimuuliza mwanadada aliyehudumu bei ya ile paketi. Alinishangaza sana kuwa inauzwa elfu mbili. Ni kwa sababu hazitoki Kilifi au Kenya. Wakati zilikuwa zinatoka Kenya, korosho zilikuwa bei ndogo na ni lishe nzuri. Tangu hicho kiwanda kivunjike, hakuna mtu amefuatilia. Namshukuru ndugu yangu Owen kwa kufufua hili suala. Hiki kiwanda kikifufuka, maelfu na maelfu ya akina mama, wazee na vijana watapata kazi hapa. Vile vile Kenya itakuwa inaongeza mapato yake kwa njia ya ushuru. Umesikia mihadarati imezidi Pwani, ni masuala kama haya. Viwanda kama hivi vikiinuliwa na kwingine, hata wafike kule Ramisi na kufufua kiwanda cha sukari, utakuta masuala mengi yako shwari kule Pwani na kwa Wakenya wote kwa ujumla. Wenzangu wamechangia sana na singependa kuregelea. Nimeshukuru kwa kunipa fursa hii na ninaunga hii Hoja kwa dhati kabisa. Asante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda."
}