GET /api/v0.1/hansard/entries/817950/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 817950,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/817950/?format=api",
    "text_counter": 64,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Msambweni, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Suleiman Dori",
    "speaker": {
        "id": 2388,
        "legal_name": "Suleiman Dori Ramadhani",
        "slug": "suleiman-dori-ramadhani"
    },
    "content": " Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Nasimama kuchangia Hoja ambayo Mhe. Owen ameleta juu ya masuala ya korosho. Ufufuzi wa korosho ni jambo ambalo litasaidia sana sehemu ambazo kwa mara nyingi zimekuwa zikikuza mmea huu kwa muda mrefu kisha ukaachiliwa. Katika sehemu hizo, hali ya umaskini imetanda. Wale wakuzaji wamerudi chini kimaisha. Kwa hivyo, ikiwa Serikali itafufua upandaji wa korosho ninayo Imani kuwa umaskini katika sehemu hizi utapungua. Aidha, moja kwa moja, kutabuniwa ajira katika sehemu ambazo zinakuza mmea huu. Isitoshe, ikiwa ukuzaji wa mkorosho utapewa kipaumbele na uzingatiwe kama mimea mingine inayokuzwa Pwani kama vile miembe na minazi basi hata kule bandarini, ambako tunategemea pakubwa kama nchi, kutakuwa na mashehena mengi ambayo nayo yatachangia kupata mapato kwa njia ya utozaji ushuru. Mapato hayo yatatuwezesha kuendeleza sekta mbali mbali katika taifa hili. Ufufuaji wa mmea wa korosho utasaidia kuzuia uuzaji wa ardhi kwa bei duni. Katika Pwani tegemeo letu kubwa ni mimea mitatu kama nilivyosema awali: minazi, mikorosho na miembe. Ninafahamu kwamba kule Kwale hakukuzwi korosho kabisa. Hilo limesababisha umaskini mwingi kwa sababu watu hawana pato lolote la kuendeleza maisha yao. Wakaazi wa huko huuza ardhi zao kwa bei duni ili kuweza kujikimu kimaisha. Kwa hivyo, suala hili naliunga mkono nikisema tufufue mkorosho. Serikali izingatie shughuli hii ya kufufua ukuzaji wa mmea huo wa mkorosho. Tukifanya hivyo tutahifadhi ardhi ambazo zimebakia kwa shughuli ya kilimo na tutamwezesha mwananchi kujikimu na kujimiliki kibinafsi. Wizara ya Kilimo sharti iangazie ufufuzi wa viwanda vya korosho vilivyokuwepo awali, kwa mfano, kiwanda cha Kilifi. Viwanda hivi vilisaidia pakubwa sana. Sizungumzii kiwanda cha Kilifi peke yake. Wizara ya Kilimo iweke utaratibu kiasi cha kwamba kila sehemu kunakokuzwa korosho kuwekwe viwanda, hata kama ni vidogo, vya kumwezesha yule mkuzaji ama mkulima kuuza mazao yake kwa njia ya rahisi. Ningependa kutoa mfano wa Kwale. Kiwanda cha korosho kilichoko huko ni cha watu binafsi na ndiyo maana tulionelea gavana wetu hatoweka pesa za Serikali katika kiwanda hicho. Lakini ni jukumu letu kuhakikisha kuwa tumekuza mkorosho kwa The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}