GET /api/v0.1/hansard/entries/817951/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 817951,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/817951/?format=api",
    "text_counter": 65,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Msambweni, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Suleiman Dori",
    "speaker": {
        "id": 2388,
        "legal_name": "Suleiman Dori Ramadhani",
        "slug": "suleiman-dori-ramadhani"
    },
    "content": "wingi. Itakuwa vema ikiwa Wizara ya Kilimo itatenga pato maalum la kuhakikisha kila sehemu katika nchi hii, kwa mfano, Tharaka Nithi, Pwani na kwingineko kunakokuzwa korosho kujengwe viwanda vidogo vidogo na wakulima wawezeshwe kuuza mapato yao. Kupitia Wizara ya Kilimo tunafahamu kwamba kuna mbegu maalum ambazo zimeletwa ambazo wakulima watapatiwa. Mbegu hizo ni za mkorosho na mnazi. Aidha mbegu hizo zikipandwa zinakua kwa miaka mitatu. Wizara ya Kilimo ikifaulisha upeanaji wa mbegu hizo, tuna imani kuwa katika miaka mitatu hali ya maisha ya watu wetu itabadilika. Nikimalizia, Mhe. Mbogo wa Kisauni amesema kwamba korosho zinaliwa katika ndege lakini nataka nitofautiane naye. Huyu rafiki yangu mara nyingi anapanda ndege ya Fly 540 na hakuna korosho inapeanwa pale. Kwa hivyo, hayo si maneno ya ukweli. Mimi naunga mkono Hoja hii ya korosho. Asante sana."
}