GET /api/v0.1/hansard/entries/817965/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 817965,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/817965/?format=api",
    "text_counter": 79,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Zao hili watu wanalizungumzia tu juu ya korosho za kula lakini mmea mzima kwa ujumla una manufaa. Mkorosho hutoa tunda ambalo lingekuwa saa hizi badala ya watu kwenda hotelini na kunywa juisi ya pensheni na miparachichi, wangekuwa wanakunywa kinywaji cha bibo. Lile tunda lake linaitwa bibo. Linatoa kinywaji kizuri sana ambacho kina manufaa kuliko hivi vinywaji tumevizoea. Pia mmea huu, mbali na ile inayoliwa huwa inatoa mafuta. Lile ganda lake lina uwezo wa kusagwa na kutoa mafuta ambayo yana maana nyingi. Tulijulishwa hapo awali kuwa yalikuwa yakitumiwa kama mafuta ya kuendesha ndege. Sijui kama utafiti huo ulithibitishwa lakini zao hili linatoa mafuta ya maana."
}