GET /api/v0.1/hansard/entries/817968/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 817968,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/817968/?format=api",
    "text_counter": 82,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Mzao wa korosho hauko Kilifi peke yake. Uko maeneo ya Lamu na ukija maeneo ya Kwale, hasa katika maeneo yangu ya Bunge ya Matuga, utakuta ulikuwa mzao ambao ulikuwa unatiliwa maanani. Ilipofika miaka ya themanini, ukaweza kujengewa kiwanda cha pili cha kutengeneza korosho. Kiwanda hiki hakikuweza kumalizika kwa sababu ni wakati huo huo ambapo pia zao la korosho liliweza kushuka chini kwa sababu ya bei. Baadaye, kile kiwanda cha Kilifi kilibomolewa, wakulima wakakosa soko na wakuzi wakaacha kulikuza zao hili."
}