GET /api/v0.1/hansard/entries/817969/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 817969,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/817969/?format=api",
"text_counter": 83,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Kwa hivyo, ni jukumu letu kama viongozi kusaidiana kuona kwamba Serikali inafufua viwanda hasa kile cha Kwale. Tuangalie kwamba maeneo yale ya Kwale hasa Eneo Bunge la Matuga, hakuna kiwanda kingine chochote kinachoweza toa ajira. Moja kwa moja, labda huenda hii ikawa inachangia kwa wale barubaru ambao hujiunga na magenge mbalimbali mpaka yale ya Al Shabaab, ambayo watu huyaogopa huwa yanatoka maeneo ya kule kwangu. Hii ni kwa sababu hakuna mahali ambapo vijana wanaweza kupata ajira ilhali uwezakano upo ikiwa tutafufua ukuzaji, upandaji na hatimaye kiwanda ambacho kiko Kwale katika Eneo Bunge langu la Matuga."
}