GET /api/v0.1/hansard/entries/817976/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 817976,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/817976/?format=api",
    "text_counter": 90,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Matuga, ANC",
    "speaker_title": "Hon. Kassim Tandaza",
    "speaker": {
        "id": 13287,
        "legal_name": "Kassim Sawa Tandaza",
        "slug": "kassim-sawa-tandaza"
    },
    "content": " Sio pizza ni bixa . Mmea huu unatumika kwote ulimwengu na unatumika kwa chakula. Ni mmea wenye thamani. Pia, ni jukumu la Serikali kuona kuwa mmea huu unakuzwa na kiwanda kile kinapatiwa nguvu ili kiweze kutoa ajira kwa vijana wetu. Ni jukumu la kila Mkenya hasa kupitia utafiti, maana saa hizi watu wakizungumza ni kama wanafikiria labda korosho ziko Pwani peke yake. Tunajua kwamba utafiti uliofanyika hapo nyuma ulidhihirisha kwamba mmea huu wa korosho unaweza kufanya vizuri maeneo mengine ya Kenya hasa maeneo ya kule Tharaka Nithi ambayo ni karibu na Meru. Hali kadhalika, suala la mnazi pia limedhihirishwa kwamba sio Pwani peke yake lakini hata maeneo mengine ya Tharaka Nithi na Meru. Kwa hivyo tukizungumzia mmea huu, ninawaomba viongozi wenzangu tulitilie mkazo jukumu hili. Tuweze kulipongeza kwani sio suala la watu wa Pwani peke yake lakini ni suala ambalo lina uwezo wa kusaidia nchi nzima na vijana wetu katika lile janga kubwa la kukosa ajira tukiona kwamba ajenda ya viwanda inapewa nguvu kupitia mazao haya. Kwa hayo mengi, ninaunga mkono. Nimetanguliza. Siungi mkono peke yake kwa sababu zao hili linaniathiri kwa The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}