GET /api/v0.1/hansard/entries/818646/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 818646,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/818646/?format=api",
    "text_counter": 445,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu CWR, JP",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Ruweida Obo",
    "speaker": {
        "id": 786,
        "legal_name": "Ruweida Mohamed Obo",
        "slug": "ruweida-mohamed-obo"
    },
    "content": " Ahsante, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii kuchangia. Ninaheshimu sana walimu kwa sababu wao ni kioo katika jamii. Tukiwa shuleni huwa tunaigiza walimu. Nimeshangazwa sana na mwalimu huyu. Sijui ni mfano gani anaonyesha wanafunzi. Najua Kenya tuna Wakristo na Waislamu wanaopendana. Haya mambo ambayo yametukia hayamo humu nchini. Huyu ni mwalimu na hilo kosa alilofanya ni yeye mwenyewe anafaa kuchukuliwa hatua za kisheria. Ikiwa kuna mwingine anachezea na kukosea heshima Biblia, naye pia achukuliwe hatua za kisheria. Hapa ametuudhi. Mimi naona hivi: Wanaiga mambo wanayoona katika mitandao. Huu ni ukoloni mamboleo. Mambo haya huku kwetu Afrika hayako. Wanaiga nchi za kizungu. Mambo hayo yanafanyika huko lakini Afrika hayafanyiki. Itakuwa vizuri awe mfano kwa wengine maana ni uhalifu amefanya. Ni kama wale wahalifu wa kigaidi wanaoharibia Uislamu jina. Nimefurahi kwamba watu wa Ijara hawakuchukua hatua mikononi mwao. Naomba mwalimu huyu achukuliwe hatua za kisheria maana si mfano mzuri analeta na huenda ikaleta matatizo zaidi. Ikiwa kuna mtu pia amekosea heshima Biblia, naye pia achukuliwe hatua za kisheria. Asante."
}