GET /api/v0.1/hansard/entries/818658/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 818658,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/818658/?format=api",
    "text_counter": 457,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu East, JP",
    "speaker_title": "Hon. Ali Sharif",
    "speaker": {
        "id": 2100,
        "legal_name": "Shariff Athman Ali",
        "slug": "shariff-athman-ali"
    },
    "content": " Asante, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Ningependa kuungana na wenzangu kulaani kitendo ambacho kilifanyika cha ukosefu wa nidhamu kwa dini zetu ambazo zimetambulika ulimwenguni huu. Ingawaje pengine Mheshimiwa na watu wake wa Garissa watalisamehe jambo hili, nataka ukubaliane na mimi kwamba mhusika mkuu ndiye anapaswa kuchukue nafasi hii ya kuomba msamaha hata si kwa jamii ya Garissa, bali kwa mwenyezi Mungu. Dini zote hizi si za binadamu ni za Mwenyezi Mungu. Hajamkosea binadamu, amemkosea Mwenyezi Mungu. Dini zote zinazotambulika, hususan zile dini ambazo zimepewa vile vitabu ambavyo vinatambulika katika ulimwengu huu, ni za Mwenyezi Mungu. Waislamu ni watu wa amani. Hatupendi vitendo kama hivi. Masikitiko yangu makubwa ni kwamba nakumbuka kunaye mama mwingine aliyefanya kitendo hiki na kukanyanga Quran. Haikupita mwezi moja wakati miguu yake yote miwili ilikuwa mikubwa na hakuweza kutembea wala kuinuka. Kwa hivyo, ni lazima tuheshimu dini zote ambazo zimetambulika na hususan ndivyo Katiba yetu inavyotuongoza kuheshimu na kutambua dini zetu."
}