GET /api/v0.1/hansard/entries/819221/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 819221,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/819221/?format=api",
"text_counter": 152,
"type": "speech",
"speaker_name": "Bura, JP",
"speaker_title": "Hon. Ali Wario",
"speaker": {
"id": 252,
"legal_name": "Ali Wario",
"slug": "ali-wario"
},
"content": " Nachukua fursa kukushukuru kwa kunipa fursa nichangie Hoja iliyo mbele yetu. Kwanza kabisa, msimamo na maamuzi yangu juu ya Hoja hii ni kwamba naiunga mkono. Nimefanya kazi pamoja na Mhe. Chepkong’a katika Bunge la Kumi na Moja kama mwenyekiti, mtunzi na mwanasheria. Ninaamini ujuzi aliyokuwa nao kutekeleza wajibu wake kama mbunge na mwenyekiti. Kama kuna taasisi katika taifa la Kenya inayoeleweka vibaya ni taasisi ya Bunge. Pengine ni kwa sababu tunatunga sheria ambazo hazifurahishi wengi ndiposa dunia imekataa kutuelewa na kuchukulia Wabunge vibaya. Mahali ninakaa kama Mbunge, ninaamini ni tume inayotoa huduma katika Bunge ndiyo inaweza kutoa fikra za wakenya na inaweza badilisha uso wetu kama viongozi wa taifa ili Wakenya waweze kutuelewa. Kwa hivyo, kiongozi kama Chepkong’a alikuwa ndani ya Bunge na anajua Bunge ni nini. Nikiwa mfano, najua sehemu mbili za shilingi. Ninajua kupata kiti na kuwakilisha wananchi hapa na pia najua kukosa. Ni muhimu Wakenya waelewa wajibu wa Wabunge wao. Sisi tumepewa wajibu muhimu wa utunzi wa sheria na usimamizi wa utendajikazi wa Serikali. Tumeondolewa wajibu muhimu na sasa tumekua taasisi ya maendeleo. Kukiwa na kifo, lazima uwe hapo, kukiwa na harusi, lazima uwe hapo, kuna mgonjwa, lazima uwe hapo. Kuna wakati fulani nikiwa Tana River, kulikua na mtu mkubwa katika Serikali na wanachi hawakuenda kwake. Matatizo yao The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}