GET /api/v0.1/hansard/entries/819222/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 819222,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/819222/?format=api",
    "text_counter": 153,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Bura, JP",
    "speaker_title": "Hon. Ali Wario",
    "speaker": {
        "id": 252,
        "legal_name": "Ali Wario",
        "slug": "ali-wario"
    },
    "content": "yalikua yanaenda kwa Mbunge. Zama zile nilikua nikiongea juu ya Sarah Serem kuwa amevunja sheria kulia, kusini, kaskazini na kati kwa sababu ya kudhulumu haki ya Wabunge. Mhe. Chepkong’a atakapokuja katika tume hii, atajua wajibu wa Wabunge na bila shaka atasimama kutetea haki yetu. Kwa sababu wazungumzaji ni wengi, ningependa kufupisha mchango wangu. Nina ombi kwako kwa mwenyekiti wa tume ya huduma ya Bunge. Kipengele cha saba cha Katiba, kinatambua Kiswahili kama lugha rasmi na lugha ya taifa. Kipengele 77 cha Kanuni ya Bunge kinatambua Kiswahili kama lugha rasmi na lugha ya taifa. Lakini, kanuni ya Bunge imeandikwa kwa kizungu, Katiba ya taifa imeandikwa kwa kizungu, ratiba ya kikao cha Bunge cha siku imeandikwa kwa kizungu. Inabidi sasa uchukue Katiba, Kanuni za Bunge, ratiba ya kikao cha Bunge na uanze kutafsiri kwa lugha ya Kiswahili badala ya kuangalia kipengele na kukizungumzia. Najua katika Bunge la Kumi na Moja na Bunge la Kumi tume inayotoa huduma kwa Bunge imefanya kazi kubwa. Tunawapa kongole, tunawapongeza. Lakini lazima tuwe na vyombo vyakutuwezesha kama wazungumzi wa Kiswahili ili tuweze kuchangia mada kikamilifu. Hili ni ombi na ni wajibu kwa commissoners ambao wamechaguliwa."
}