GET /api/v0.1/hansard/entries/820227/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 820227,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/820227/?format=api",
    "text_counter": 345,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Cherangany, JP",
    "speaker_title": "Hon. Joshua Kutuny",
    "speaker": {
        "id": 61,
        "legal_name": "Joshua Serem Kutuny",
        "slug": "joshua-kutuny"
    },
    "content": " Asante sana, Naibu Spika wa Muda. Nashukuru sana kwa nafasi hii umenipa nichangie na kuzungumzia suala hili la mazingira. Kwanza, nitachukua fursa hii kukashifu Serikali kwa jinsi ilivyofurusha watu ambao ni akina yahe kwa makazi yao. Nitasema kwa nini ni makazi yao. Wale watu wameishi pale. Kule Mau ndio kwao. Sio kwao kimakosa. Serikali kuwa na tabia ya ndumakuwili ndiyo imenipatia nafasi hii kuikashifu licha ya kuwa mwanachama wa Serikali hii. Wamama wameumia. Wakongwe wamenyeshewa. Watoto zaidi ya 4,000 wameachwa bila masomo. Shule zaidi ya sabini zimebomolewa. Watu wamekosa maji safi. Wale wagonjwa wamekosa dawa. Swali ambalo ningependa kuuliza ndani ya Bunge ni kwamba tangu tukio hili la watu kufurushwa Mau litokee, hatujaona Waziri wa Mazingira na Misitu akitembea kule. Hatujaona Waziri wa Maji, Waziri wa Ardhi ama Waziri ambaye anashughulikia majanga akitembea kule."
}