GET /api/v0.1/hansard/entries/820229/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 820229,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/820229/?format=api",
    "text_counter": 347,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Cherangany, JP",
    "speaker_title": "Hon. Joshua Kutuny",
    "speaker": {
        "id": 61,
        "legal_name": "Joshua Serem Kutuny",
        "slug": "joshua-kutuny"
    },
    "content": "kuhifadhiwa lakini tunataka ifanywe kisheria. Pale Mau kuna laini mbili. Kuna laini ya kwanza ambayo Mhe. Raila Odinga aliibuni wakati alikuwa Waziri Mkuu. Kuna laini nyingine iliyobuniwa na Rais Uhuru Kenyatta aliposhika usukani. Serikali ambayo iko mamlakani ni ya Uhuru Kenyatta. Tunasimama na uamuzi wa Rais Uhuru Kenyatta kwamba mpaka ndio huu. Kwa hivyo, tunataka kuuliza ni nani huyo ameenda kinyume na msimamo wake Rais Uhuru Kenyatta akafurusha watu. Wale watu wanaofurushwa hawako ndani ya msitu. Wako kwa makazi yao na inajulikana. Kuna kitu ambacho kinaitwa kwa kimombo cutline . Kwa hivyo, mimi ningependa Bunge lizungumzie suala hili kimakini. Nimesikia hapa kila Mhe. anaisifu Kamati ambayo imefanya kazi. Mgala muue lakini haki yake umpatie. Kamati haijazingatia matatizo ya wale watu ambao walifurushwa. Watapelekwa wapi? Je, watapewa sehemu badala? Hilo ndilo jambo ambalo linatukera sisi."
}