GET /api/v0.1/hansard/entries/820230/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 820230,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/820230/?format=api",
"text_counter": 348,
"type": "speech",
"speaker_name": "Cherangany, JP",
"speaker_title": "Hon. Joshua Kutuny",
"speaker": {
"id": 61,
"legal_name": "Joshua Serem Kutuny",
"slug": "joshua-kutuny"
},
"content": "Mimi ni kati ya Wabunge ambao wanatoka maeneo ambayo chemichemi ya maji katika taifa la Kenya ipo. Huko ni mlima wa Cherangany. Mmoja wa wanakamati amesema kwamba walitembea katika kila msitu Kenya nzima lakini hawakufika kwetu. Kamati hii haikutembea Kenya nzima. Walienda sehemu mmoja na wakatengeneza Ripoti kulingana na fikra zao. Hawakutembelea Wakenya wote. Kwa hivyo, Kamati hii haijafanya kazi bora. Kile ambacho nataka kusisitiza ni kwamba hatuzungumzi mambo ya kuhifadhi misitu kwa mara ya kwanza leo. Misitu ipo. Tukielezwa kwamba kuna mito ambayo inanyauka Aberdare ama Mkoa wa Kati katika Taifa la Kenya, ina uhusiano ngani na Mau? Hilo ndilo swali. Mto wa Nairobi hapa ukikauka, una uhusiano ngani na Mau? Tukiambiwa mito inakauka kule Kisumu ambapo hata Waheshimiwa hawajapanda miti hata siku moja, inauhusiano ngani na Mau? Nilitembea kule na nikaona ni jangwa. Kunakatwa miti kila siku. Sisi tunahifadhi mazingira lakini tunapata faida gani? Tunapigwa na kufurushwa."
}