GET /api/v0.1/hansard/entries/820430/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 820430,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/820430/?format=api",
    "text_counter": 144,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Barabara ambayo inatoka Mwingi inaunganisha sehemu yangu ya Tana River na Garissa pia. Huwa ninasafiri katika barabara hiyo kila wakati ninapoelekea Kaunti ya Tana River. Kwa hakika, barabara hiyo iko katika hali ya kusikitisha sana hasa sehemu ya Nguni kuelekea Bangali. Sehemu hiyo iko katika hali mbaya zaidi. Wakati mwingi, ajali zinatokea katika sehemu hizo. Vijana wengi husafiri kwenda kujifunza na kujionea mambo halisi yalivyo katika sehemu tofauti tofauti. Hata hapa bungeni, wanafunzi wengi huja. Hata sasa kuna vijana kutoka Tana River ambao wanasafiri kuja hapa Bunge kupitia barabara hiyo. Sehemu hiyo ya barabara haifai kupitiwa na magari. Ni wakati halisi kwa wale wanaohusika na barabara hiyo kuirekebisha. Hii ni kwa sababu tunazungumza mambo ya ajali ambayo imefanyika na waathiriwa wako hospitalini. Hawa ni vijana wa watu masikini ambao ni tumaini letu kwa siku zijazo. Walipata ajali na familia moja iliwapoteza vijana wawili. Hiyo ni uchungu sana na haya ni mambo ambayo tunaweza kuepukana nayo. Maji yakimwagika hayazoleki tena. Kupitia Seneta ambaye ni rafiki yangu---"
}