GET /api/v0.1/hansard/entries/820436/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 820436,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/820436/?format=api",
    "text_counter": 150,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. (Dr.) Zani",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13119,
        "legal_name": "Agnes Zani",
        "slug": "agnes-zani"
    },
    "content": "Ahsante sana, Bw. Spika, kwa nafasi hii. Ningependa kuwaambia pole, wale ambao walipoteza wapendwa wao, haswa ile familia ambayo tuliona katika magazeti ambayo imepoteza watahiniwa wawili. Hili ni jambo la huzuni lakini sio jambo jipya. Ni jambo ambalo limezungumziwa mara nyingi lakini hakujakuwa na suluhu ambayo imeweza kupatikana ndio hizi ajali zisifanyike. Wengi wamezungumza juu ya sera ambayo ni muhimi, na sera zipo. Sera moja muhimu ambayo ilikuwa imewekwa ni kwamba; ni lazima basi ambalo linapeleka wanafunzi pahali fulani liendeshwe baina ya masaa fulani; halitakikani kuendeshwa usiku. Jambo la pili ni kwamba, dereva ambaye anaendesha hilo basi, ni lazima awe na mwenzake. Mimi nilijiuliza; ‘kwani, basi hilo ama dereva huyo hangeweza kupumzika ama hawakuwa na mpangilio mwingine ambao ulikuwa umewekwa kuhakikisha ya kwamba wanafunzi hao wanalala pahali fulani?’. Hii ni kwa sababu imesemekana ya kwamba, ajali ilifanyika kwa sababu ilikuwa ni usiku. Ajali hiyo ilifanyika kwa sababu dereva aliacha barabara kwa sababu kulikuwa na kilima ambacho kilimzuia kuona barabara vizuri. Wengi wetu ambao tumekuwa katika barabara, mara nyingi tukifika nyumbani ni lazima tumshukuru Mungu. Huwa tunastaajabu ya kwamba tumefika salmini, kwa sababu ni maajabu ukifika bila ajali. Barabarani, utapata wale ambao wamebeba mizigo mikubwa au mtu ambaye ameingia barabarani katika kona bila kuzingatia usalama wa wenzake. Itakuwa vizuri tukiangalia sera ambazo tumeziweka. Nilisikia kwamba sera hizi zitaangaliwa kuhakikisha ya kwamba zimefuatwa. Nafikiria ya kwamba dereva yule amepelekwa kortini na akifungwa, itakuwa ni dereva mmoja tu. Lakini, ni kwa nini sera zivunjwe? Na kama zimevunjwa, kwa nini ziendelee kuwekwa? Lazima tujiulize na tuhakikishe ya kwamba mambo kama hayo hayafanyiki. Kama ni sera imewekwa, lazima sera ifuatwe na mtu ambaye hatafuata hiyo sera anatikiwa kuadhibiwa vilivyo. Kuna sera nyingi ambazo zinawekwa, kwa mfano, mabasi za shule yapakwe rangi moja. Watu kwa wakati huu wanazungumza kuhusu sare za wanafunzi ambazo zinaonyesha shule wanakotoka. Lakini, ninafikiri ya kwamba tutapata shida kwa sababu sisi kwa mara nyingi tunazungumza juu ya kutunga sera bila kuhakikisha ya kwamba zimefuatwa. Kwa mara nyingine, katika historia ya Kenya, tumeingia katika shida kwa sababu ya ajali kubwa ambayo imetendeka kwa sababu ya kutokufuata sera."
}