GET /api/v0.1/hansard/entries/820440/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 820440,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/820440/?format=api",
"text_counter": 154,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Ahsante sana, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii kuchangia arifa iliyoletwa na Seneta wa Kitui; Sen. Wambua. Ninachukua fursa hii kutoa rambirambi zangu binafsi na za watu wa Mombasa kwa watu wa Kitui kutokana na mkasa huu wa ajali uliotokea majuzi. Fikra zangu na maombi yangu yote yako kwa familia hususan ile familia ambayo ilipoteza watoto wawili kutokana na hiyo ajali. Mwenyezi Mungu awaweke mahala pema peponi. Mhe. Spika, swala la ajali barabarani limekuwa donda ndugu katika nchi yetu ya Kenya. Tumeona hapo nyuma mwezi wa nne kulikuwa na ajali zilizotokea na watu wengi wakapoteza maisha yao na mpaka sasa NTSA haijafanya jambo lolote kuzuia ajali hizi. Kuna maswala ya shirika la Transport Licensing Board (TLB) na maafisa wa polisi wa Idara ya Usafiri ambao wanasimama katika kila kaunti kupokea hongo, wakati mwingine ili kuyaruhusu magari ya abiria kubeba zaidi. Pia, magari ambayo yana makosa madogo madogo ya trafiki yanakubaliwa kuendelea na safari. Mhe. Spika, hayo yote yanaweza kukoma iwapo serikali itakaa ngumu na kuhakikisha ya kwamba sheria za barabarani zimedumishwa. Kwa mfano, haiwezekani gari litoke Mombasa na Saa Tano ya usiku likibeba watoto wadogo ambao wanatakiwa wakati kama huo wawe wamelala ili waweze kupumzika na safari na machovu mengi. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}