GET /api/v0.1/hansard/entries/820442/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 820442,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/820442/?format=api",
    "text_counter": 156,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Ni lazima serikali ijifunge kibwebwe hususan mwezi huu wa nane ambapo kuna safari nyingi za wanafunzi kutoka sehemu moja kwenda nyingine. Jana, nilibahatika kuona zaidi ya magari kumi ya wanafunzi. Kulikuwa wanafunzi wadogo sana ambao hawawezi kwenda masaa 12 bila kupumzika. Mhe. Spika, ninachukua fursa hii kuomba Serikali kuhakikisha ya kwamba sheria za barabarani zinadumishwa. Hayo yatafanyika iwapo Serikali itakaa ngumu na maafisa wa trafiki na NTSA kuhakikisha ya kwamba sheria zinadumishwa. Acha safari zichelewe lakini watoto waweze kufika salama."
}