GET /api/v0.1/hansard/entries/821436/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 821436,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/821436/?format=api",
    "text_counter": 38,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Matungu, ANC",
    "speaker_title": "Hon. Justus Makokha",
    "speaker": {
        "id": 13430,
        "legal_name": "Justus Murunga Makokha",
        "slug": "justus-murunga-makokha-2"
    },
    "content": " Asante sana, Mhe. Spika. Naunga mkono Ombi hili kuhusu mateso ambayo wakulima wetu wanapitia. Ni kweli mkulima wetu anapitia mateso mengi kwa sababu unapolima shamba lako, unatarajia kupata mavuno kama vile sisi tunavyokuja Bunge tunatarajia tupate mshahara wetu. Wakulima wa Kenya wanaendelea kupata mateso awe ni mkulima wa miwa au wa mahindi kwa sababu hapati mavuno ambayo anatarajia. Hili ni jambo ambalo tunafaa kulichukulia maanani kwa sababu mkulima akilima shamba lake anategemea mazao hayo kufanya kazi, kwa mfano, kulipia watoto wake karo ya shule na kulima shamba tena arudishe mazao ndani. Si vyema Serikali tukufu iwache wakulima kama hao wateseke. Kwa mfano, tulikuwa sehemu ya Eldoret mwezi wa tatu mwaka huu na kusema kweli tulipata wakulima wakiwa na malalamiko ya kutolipwa na huo ndio wakati walikuwa wanajitayarisha kulima tena mashamba yao. Ingawaje Serikali ilitoa pesa kwa kiwango kikubwa na ikaongeza bei ya mahindi, unapata kwamba anayenufaika kwa kupata mapato kutoka kwa malipo haya si mkulima wa kawaida. Unakuta kwamba ni watu wengine waliagiza mahindi kutoka nje ya nchi hii ndio waliopeleka mazao hayo kwa stoo hizi na wakanufaika badala ya mkulima wa kawaida. Hili si jambo zuri na ninawaomba Wabunge wenzangu wachukulie jambo hili kwa hali ambayo inatakikana ili mkulima asiendelee kupitia mateso anayoyapitia. Kwa mfano, wakati huu tunapoongea, sio mkulima wa mahindi tu anayeteseka peke yake lakini hata mkulima wa miwa pia anateseka. Unakuta kuwa hata viwanda vyetu vinaanguka kwa sababu ya hali hii na si vyema."
}