GET /api/v0.1/hansard/entries/821902/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 821902,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/821902/?format=api",
    "text_counter": 115,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Likoni, ODM",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Mishi Mboko",
    "speaker": {
        "id": 874,
        "legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
        "slug": "mishi-juma-khamisi"
    },
    "content": "Tumeona wasichana wengi wadogo wakinajisiwa na wale wa kiume wakilawitiwa. Mara nyingi uovu huu hutendwa na jamaa wa karibu sana katika jamii zetu. Makaazi haya tunayozungumzia yakitengenezwa, watu waliodhulumiwa watapata mahali pa kupumzika na kupata ushauri. Aidha, watapatiwa matibabu na mwelekeo mwema wa kurudia maisha yao ya kawaida. Tendo la kunajisi ama kulawiti humpa anayekosewa hofu na kumfanya ajihisi si binadamu wa kawaida tena. Wakati mwingine utapata watu wakiwakejeli na kuwashushia hadhi waathiriwa wa matendo hayo maovu. Kwa sababu hiyo, ni wazo zuri kwamba waathiriwa wapate makaazi ambamo watatuliza mioyo na akili zao. Jambo hili si gumu kutekeleza katika nchi yetu ya Kenya. Sasa hivi tuna hazina ya National Government Affirmative Action Fund. Hazina hii inasimamiwa na akina mama 47 ambao wanawakilisha kaunti za taifa letu. Kutoka kwenye hazina hiyo, tunaweza kupata pesa zitakazotumika kutengeneza Rescue Centres ambazo Mhe. Jessica Mbalu amezungumzia katika Hoja yake. Vile vile kuna misaada mingi kutoka mashirika ambayo sio ya Serikali. Kuna wafadhili wetu nchini ambao wanataka kusaidia katika kukabiliana na dhuluma kama hizi tulizozitaja. Ingawa hivyo, mara nyingi tunapata habari kwamba pesa zimetumiwa kwa njia ya kiholela na pia haziwafikii waliolengwa, yaani waliodhulumiwa."
}