GET /api/v0.1/hansard/entries/821903/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 821903,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/821903/?format=api",
"text_counter": 116,
"type": "speech",
"speaker_name": "Likoni, ODM",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Mishi Mboko",
"speaker": {
"id": 874,
"legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
"slug": "mishi-juma-khamisi"
},
"content": "Tukishatengeneza makao haya maalum ya waathiriwa, itatulazimu kuweka mikakati na mifumo makhususi ya kuhakikisha matumizi mazuri ya pesa. Hivyo, tutahakikisha pesa zimewafikia waliolengwa. Makao hayo pia yatatuwezesha kupata takwimu sahihi kuhusu visa vya dhuluma dhidi ya wanyonge. Sasa hivi kuna watu wengi ambao wanapata matatizo lakini wamejificha na wamenyamaza. Ni kwa sababu hawajui watapata afueni kutoka wapi. Hawajui ni taasisi gani ambayo inaweza kuwasaidia kwa njia ambayo haitawaibisha ama kuwakejeli."
}