GET /api/v0.1/hansard/entries/821929/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 821929,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/821929/?format=api",
"text_counter": 142,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa CWR, ODM",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Asha Hussein",
"speaker": {
"id": 13262,
"legal_name": "Asha Hussein Mohamed",
"slug": "asha-hussein-mohamed"
},
"content": " Ahsante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Kwanza, naunga mkono Mhe. Jessica Mbalu kwa kuleta Hoja hii. Naiunga mkono kwa sababu itakuwa vyema Serikali itakapoweza kutenga pesa hizi kujenga vituo hivi vya ushauri dhidi ya ubakaji na dhuluma za kijinsia. Tunaona watoto wetu wakiteseka sana katika jamii. Wanapopata matatizo, kudhulumiwa na kurudi nyumbani, wengine huenda wakarukwa na akili. Kuna wale wamerukwa na akili kwa sababu ya ubakaji na hivyo, kupoteza hamu ya kuishi katika jamii. Serikali itakapotenga pesa hizi na vituo hivi kujengwa ili hao watoto wetu na akina mama wanaodhulumiwa waweze kupata ushauri na kuondoa unyanyapaa katika jamii, itakuwa heri. Mtoto anapobakwa ama mama kupigwa na mumewe kupita kiasi, hawa hujitenga katika jamii; hata jamii inawatenga wadhulumiwa hao. Kwa hivyo, vituo hivi vya ushauri vitawawezesha wao kupata ushauri mzuri na kuondoa ule unyanyapaa katika jamii na wao kuweza kurudi kufanya kazi zao kama kawaida. Kwa hivyo, naunga Mkono Hoja hii na nasihi Serikali itenge fedha ili vituo hivi vijengwe na waathiriwa waweze kupata huduma hii. Ahsante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda."
}