GET /api/v0.1/hansard/entries/823415/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 823415,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/823415/?format=api",
    "text_counter": 160,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Nyali, Independent",
    "speaker_title": "Hon. Mohamed Ali",
    "speaker": {
        "id": 13455,
        "legal_name": "Mohammed Ali Mohamed",
        "slug": "mohamed-ali-mohamed"
    },
    "content": " Shukrani sana Mhe. Naibu Spika wa Muda. Langu ni kuunga mkono Hoja hii na kupendekeza kwamba Wizara ya Elimu. Sayansi na Teknolojia iweze kuhakikisha kwamba walemavu wana nafasi katika taifa hili. Sisi Wabunge tunapata shida sana wakati tunapotembelewa na Wakenya wenzetu ambao ni walemavu katika afisi zetu. Ninakotoka katika Kaunti ya Mombasa, kuna visa kama hivyo vingi sana katika afisi yangu. Ni vigumu kuwasaidia kwa sababu Serikali haijaekeza wala kuwafikiria watoto walemavu hasa upande wa kuwapatia elimu bora katika shule za chekechea, msingi, upili na hata chuo kikuu ili waweze kupigania nafasi zao kama Wakenya wengine. Mighairi na hayo, vile vile tunaomba wawe na hospitali zao ambazo zitaweza kukimu mahitaji yao. Kwa sababu ukiwaweka pamoja na Wakenya wengine wa kawaida wasio walemavu, patakuwa na matatizo chungu nzima."
}