GET /api/v0.1/hansard/entries/823416/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 823416,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/823416/?format=api",
    "text_counter": 161,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Nyali, Independent",
    "speaker_title": "Hon. Mohamed Ali",
    "speaker": {
        "id": 13455,
        "legal_name": "Mohammed Ali Mohamed",
        "slug": "mohamed-ali-mohamed"
    },
    "content": "Shule ambazo zipo nchini kuwahudumia ni chache sana. Mimi ninajua shule mbili pekee. Ile Shule ya Thika ya vipofu na Joy Town ambayo iko Kisumu. Sharti tuwe na shule spesheli katika kila kaunti ili tuweze kusaidia hawa walemavu ambao ni Wakenya wenzetu. Demokrasia tunayopigania ni ya kuleta usawa kwa kila Mkenya. Hizi shule zinahitaji walimu na bajeti. Waalimu ni haba. Ni kweli kwamba waalimu wanaoweza kukidhi mahitaji ya hawa wanafunzi ni wachache mno. Ni lazima Serikali ihakikishe kuna walimu wanapokea mafunzo spesheli ya kuangalia watoto hawa. Ningetaka Serikali itoe bajeti kubwa sana kwa walemavu kwa sababu hawana nguvu kama Wakenya wengine. Wawekewe bajeti ambayo itawafaa. Ninaposema bajeti ninazungumzia suala kama karo na basari ambazo tunapeana kwa shule zetu. Wahakikishiwe kuwa bajeti yao imeongezwa kwa sababu wao ni tofauti kabisa. Vitu ambavyo wanahitaji ni tofauti na vitu ambavyo Mkenya wa kawaida anahitaji."
}