GET /api/v0.1/hansard/entries/823494/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 823494,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/823494/?format=api",
    "text_counter": 239,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kilifi CWR, ODM",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Gertrude Mwanyanje",
    "speaker": {
        "id": 13245,
        "legal_name": "Gertrude Mbeyu Mwanyanje",
        "slug": "gertrude-mbeyu-mwanyanje"
    },
    "content": " Asante, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Nimesimama kuunga mkono Hoja hii. Nikiwa Mpwani na Mama wa Jimbo la Kilifi, Hoja hii ni ya muhimu kwa watu wote wa Pwani na maeneo yote yanayokuza mmea wa mnazi. Tukikueleza kwa ufasaha, mmea huu ni muhimu kuliko mimea mingine yote ninayoijua kama mtu atokaye kule Kilifi. Mmea huu una faida. Aliyeleta Hoja hii amesema faida za mmea huu ni zaidi ya 100. Kuweka pesa za kufidia wakulima wa mnazi walioathirika kwa ukame kule Kilifi na Jimbo la Pwani ni jambo muhimu. Kwa sababu ya mmea huu, wakale wetu wanatuangalia kwa jicho baya manaake tumedhuru mmea na faida zake – haswa, pombe ya mnazi ama juisi inayotoka kwa mnazi ni kitengo muhimu sana katika jamii ya Wapwani. Unavyoniangalia, siwezi kutolewa mahari, wala sikutolewa mahari, hadi pombe ya mnazi ipelekwe kwa babangu kwanza, wabariki ndipo mahari kama pesa itolewe. Faida za mmea wa mnazi katika Jimbo la Pwani, na haswa Kilifi, imekuwa tegemeo kubwa sana kwa wananchi wa kwetu. Wengi tumelelewa na kulipiwa karo ya shule na akina mama zetu kutokana na mauzo ya mnazi. Hivi sasa, mangwe nyingi, ama sehemu ambako pombe ya mnazi huuzwa, zimefungwa. Akina mama wanateseka kwa sababu hawana bidhaa ya kuuza. Unavyotuona, akina mama wa Pwani, ngozi zetu zinameremeta. Hii ni kwa sababu ya mafuta ya nazi. Hatutumii mafuta ya jelly zozote. Twatumia mafuta ya nazi. Ndiposa utaona wanaume wengi wa bara wakienda kule Pwani ni mpaka watoke na bibi wa Kipwani. Ni kwa sababu bidhaa hizi zatufaa. Fagio zinazotumika Kenya na nchi za nje zinatoka kwa bidhaa ya mnazi. Twatumia mbao za mnazi kuezeka paa za nyumba zetu. Ukienda katika ufuo wa bahari, utapata hoteli nyingi hazijawekwa paa la mabati; zimewekwa paa la makuti. Ni bidhaa ya mnazi. Kulipokuwa na ukame, minazi mingi ilikauka. Twaomba Serikali, mti huu ni muhimu kuliko majani chai na kahawa. Hata mti wa miraa ulipewa Kshs1 bilioni ili wakulima wawekeze. Mti wa mnazi una faida nyingi sana. Vitu vya urembo kama vile bangili na vipuli utavipata ukifika Pwani. Hivi vinatokana na bidhaa ya mnazi. Lile tui la nazi yenyewe kwa vyakula vyetu, utatuona twang’ara. Hata Mhe. Mwashetani yuko vile alivyo kwa sababu ya vyakula vinavyopikwa na nazi."
}