GET /api/v0.1/hansard/entries/823505/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 823505,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/823505/?format=api",
"text_counter": 250,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kaloleni, ODM",
"speaker_title": "Hon. Paul Katana",
"speaker": {
"id": 13357,
"legal_name": "Paul Kahindi Katana",
"slug": "paul-kahindi-katana-2"
},
"content": " Asante, Mhe Naibu Spika wa Muda. Nasimama kuchangia Hoja hii. Mti wa mnazi ni muhimu sana katika jimbo la Pwani na Kenya nzima. Lakini, kwa muda mrefu, mti huu haujatiliwa maanani na Serikali. Mti huu ukitumika vizuri, unaweza kuinua maisha ya wapwani, Kenya nzima na Serikali inaweza kupata ushuru mwingi. Watu wa Pwani na haswa kule nitokako Kaloleni na kijiji ambako ninatoka kinaitwa Makomboani, wameathirika sana na ukame ambao ulikua mwaka wa 2016/2017. Ukame huu umechangia umasikini katika maeneo yetu. Mti huu unatumika kwa uchumi wa watu wa Pwani. Baada ya ukame mmea huu ulipotea. La kushangaza ni kwamba hakuna hata kiwanda kimoja kimetengenezwa ili kusaidia wakazi wa Pwani. Kwa wakati huu bidhaa nyingi kama vile nazi zinanunuliwa kwa bei duni na zinapelekwa katika nchi jirani ya Tanzania, kwa sababu hapa nchini, hakuna kiwanda cha kutengeneza mazao ya mnazi. Watu wengi wakitaja mnazi, walikua wanataja ile pombe peke yake. Wanasahau kuwa, mti huu una mazovu mengi zaidi ya mia moja. Nazi inatumika kupikia chakula. Chakula hiki ni kizuri kwa sababu ni cha kitamaduni na hakina kemikali na kinasaidia kuzuia ugonjwa wa saratani. Hakuna kemikali ambayo inatiwa kwa nazi."
}