GET /api/v0.1/hansard/entries/823506/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 823506,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/823506/?format=api",
"text_counter": 251,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kaloleni, ODM",
"speaker_title": "Hon. Paul Katana",
"speaker": {
"id": 13357,
"legal_name": "Paul Kahindi Katana",
"slug": "paul-kahindi-katana-2"
},
"content": "Pia, kama ulivyoambiwa, utamaduni wetu kama watu wa mijikenda, tumetumia sana mti wa mnazi. Huwezi oa ama kutoa mahari kabla pombe ya mnazi kutumika. Pia, tunaona kuwa Serikali imetumia mabilioni ya pesa kuagiza mafuta ya nazi kutoka nje, ilhali, tunayo miti ya kutosha ya kutoa mafuta ya nazi. Serikali inatakikana ichukue jukumu la kufidia hawa wakulima ambao wamepoteza minazi mingi kwa sababu ya kiangazi ili waweze kusaidika kupeleka watoto wao shuleni na wajikimu kimaisha. Kwa hivyo, tunaomba Bunge hili lipitishe Hoja hii na lihakikishe kwamba Serikali inatengeneza ama inaegemea upande wa viwanda ili wananchi na wakazi wa Kilifi na Pwani nzima waweze kufaidika."
}