GET /api/v0.1/hansard/entries/823509/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 823509,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/823509/?format=api",
"text_counter": 254,
"type": "speech",
"speaker_name": "Lungalunga, JP",
"speaker_title": "Hon. Khatib Mwashetani",
"speaker": {
"id": 2163,
"legal_name": "Khatib Abdallah Mwashetani",
"slug": "khatib-abdallah-mwashetani"
},
"content": " Asante sana, Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii ili niweze kuchangia Hoja hii. Kwanza kabisa ningependa kutoa shukurani na kumshabikia Mhe. Owen Baya na kumpa kongole kwa kuja na wazo hili. Hili ni jambo ambalo linajulikana kuwa mmea wa mnazi mbali na kuwa una faida yake ya kindani, ukiangalia mandhari yake inarembesha sehemu iliyopandwa. Iwapo mnazi utapatiwa nguvu ya kupandwa kwa teknolojia ya kisasa – na nikisema hivyo ninamaanisha Serikali iwekeze kwa mmea huu - basi katika kuchangia katika uchumi wa Kenya itakuwa ni nguvu moja. Mbali na kuwa sasa hivi ni mmea unaomea katika sehemu ambayo tumekuwa na umaskini muda mrefu, pengine kwa sababu nyingi mbalimbali za uongozi, kusahauliwa, ukame... Hivi vyote vinachangia kuathiri uchumi. Sasa hivi katika hali ile, mnazi unachangia karibu Kshs3.2 bilioni, lakini ukipatiwa nguvu za kiteknolojia na utafiti, unaweza kutoa zaidi ya Kshs13 bilioni. Ikiwa Pwani peke yake itaweza kuchangia katika suala kama hilo, kuwa uchumi unachangiwa kwa mwaka na Kshs13 bilioni, basi hiyo ni moja kati ya sehemu ambazo Serikali inapaswa kuwekeza. Sisi kila siku kama jamii ya Wakenya tunapigana na janga la ukosefu wa kazi. Na moja kati ya shughuli ambazo ukitembea Pwani utakuta vijana wetu na akina mama wetu wakifanya ni kuuza madafu na nazi. Kwa hivyo, inapeana ajira. Na hii ni ajira ambayo iko lakini haijategwa na Serikali. Iwapo Serikali itaingilia na itege ni kumaanisha tutapata ajira za viwanda; watoto wetu watafanya kazi kwa viwanda kutoa mafuta kama vile dada Mbeyu alivyosema. Sasa hivi Tanzania wanachukua nazi yetu na kutega lile tui, linafanywa kavu na kuuzwa. Linatengenezwa halafu linauzwa Kenya. Iwapo Serikali ya Kenya itawekeza kuhakikisha safari hii tumepata kiwanda cha kutega mti wa mnazi, basi nina hakika mpaka wakulima watakuwa na motisha ya kupanda zaidi. Ajenda moja ya Serikali ni kuhakikisha watu wote wamepata kazi. Na mnazi ni njia moja ambayo tutaweza kupata kazi. Kijiti kinachotumiwa kutolea nyama kwenye meno chatoka kwenye mnazi. Kapeti hii ambayo tumekanyaga yatoka kwenye mnazi. Makuti yale ambayo yako katika mandhara ama hoteli nzuri nzuri yatoka kwenye mnazi. Chakula tunachopikiwa Pwani kama samaki wa mipako ama wali wa nazi kinatoka kwenye mnazi. Mmea ule ule mti wake hutumika kama mbao. Kwa hivyo, ziko faida zaidi katika mnazi. Ningependa Serikali iupatie nguvu katika Pwani. Kuhusu suala hili la kazi, ningependa kukujuza kuwa katika shughuli zetu zote tunakwenda mbio kuhakikisha tumepata viwanda katika sehemu zetu. Lakini unakuta sasa Kwale tuko na kiwanda cha sukari lakini kimefungwa na hakiwezi kufanya kazi kwa sababu ya yale matatizo yaliyotoka juzi. Tuliingilia kama Wabunge, tukafanya utafiti na ripoti ikaja. Ni mwezi wa pili Kwale Sugar Company imefungwa na watu wetu wanapata taabu. Kile kiwanda kimeandika watu zaidi ya elfu tatu. Ikifika wiki ijayo nafikiri watafunga kwa sababu mbali na kuwa wanadaiwa, pia watu wetu…"
}