GET /api/v0.1/hansard/entries/823512/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 823512,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/823512/?format=api",
"text_counter": 257,
"type": "speech",
"speaker_name": "Teso North, ANC",
"speaker_title": "Hon. Oku Kaunya",
"speaker": {
"id": 13488,
"legal_name": "Edward Oku Kaunya",
"slug": "edward-oku-kaunya"
},
"content": "kufanya kazi kama mfanyakazi wa Serikali hapo mwaka wa 2000 hadi 2001. Wakulima wengi waliathirika sana. Vijana pia walipoteza nafasi za kazi nyingi. Tukiangazia mnazi, vile wasemaji wengi wamesema, ni tegemo kubwa sana la wakulima kule Pwani. Ninaunga mkono Hoja hii kwa sababu jambo hili litawaletea wakulima sio tu faida, lakini pia hali yao ya kimaisha itainuka. Kama vile ulivyosema, kule kwingine kama kaskazini mashariki tegemeo lao ni ng’ombe. Ng’ombe wanaleta chakula, malazi, maziwa na hata pesa za kuwezesha wakulima kuwalipia watoto karo za shule. Kule Pwani, hasa Kilifi ambapo nilifanya kazi wanategemea mmea huu kuwapatia “maziwa”. Kuna “maziwa’ inatoka kwa mnazi. Pia wao hutumia mnazi kwa ujenzi, haswa kuwezeka paa la nyumba. Kuna matumizi mengi ambayo yanatoka wa mmea huu. Kwa hivyo, mbali na kuwapatia faida ya kifedha, mnazi unawasaidia katika maisha yao ya kawaida; kuwawezesha kuishi maisha ya kawaida. Kwa hivyo, tukiwa na shida kama hii ambayo imetokana na ukosefu wa mvua, ni muhimu Serikali iwafidie wakulima na kuwapatia usaidizi. Pia kuna umuhimu wa kuanzisha kiwanda ambacho kinaweza kuwasaidia wakulima kupata faida zaidi. Mara nyingi wakulima wengi wanapata faida iliyo chini sana wakiuza mazao ya mimea yao. Kwa hivyo, naunga mkono kwa dhati Hoja hii na nasihi Serikali ifidie wakulima wa Kilifi ili warudie hali yao ya kawaida. Asante, Mhe. Naibu Spika kwa kunipa nafasi."
}