GET /api/v0.1/hansard/entries/823533/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 823533,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/823533/?format=api",
    "text_counter": 278,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Msambweni, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Suleiman Dori",
    "speaker": {
        "id": 2388,
        "legal_name": "Suleiman Dori Ramadhani",
        "slug": "suleiman-dori-ramadhani"
    },
    "content": " Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Nachukua fursa hii kuunga mkono Hoja ambayo imeletwa na Mhe. Baya, kuhusu fidia kwa wakuzaji wa mnazi. Tunataka tufanyie suala hili marekebisho kiasi cha kwamba fidia hii isielekee katika sehemu ya Kilifi ambayo imelengwa na aliyeleta Hoja, lakini ilenge wakulima wa mnazi wote kwa jumla katika nchi ya Kenya na hasa eneo la Pwani. Hii ni Hoja nzuri sana. Tunahitaji msukumo mkubwa kwa Wizara ya Kilimo na Mifugo. Tukiwa tunaelekeza mwelekeo wetu kulipa fidia kwa wakulima wa mnazi, ni lazima ifahamike kwamba wakuzaji wakubwa wa mnazi wanatoka sehemu ya Kwale katika eneo Bunge la Msambweni. Shamba ambalo linaitwa Ustawi wa Mswambweni lina ekari 3,800 ambazo zote zimepandwa mnazi. Vile vile, Mhe. Naibu Spika wa Muda, nataka kukujuza kuwa sio kwamba hatuna viwanda vya mnazi. Katika sehemu ya Msambweni, kiko kiwanda cha mnazi ambacho kinalinda haki za mnazi. Kiwanda hiki kinaitwa Kwale Coconut Farm. Kiwanda hiki kinalinda haki za wakulima katika kuuza mapato na mazao yao. Katika JamUhuri ya Kenya viwanda ambavyo vilikuwa vinanunua mali ya mnazi vilikuwa viwili. Kimoja kilikuwa mjini Mombasa kikiitwa Coast Coconut Plant Farm na kimekufa. Sasa kimebakia kiwanda kimoja ambacho kiko Kwale. Ni jukumu letu ikiwa tumelenga fidia tuangalie pia taratibu ambazo tutamlinda mkulima wa mnazi kupitia wizara ya kilimo ili aweze kuendeleza zao lake na apate faida zile ambazo zinatambulika zimepitia ukulima wa mnazi. Ni lazima suala la mnazi lipatiwe kipao mbele. Ni kama vile ambavyo wiki zilizopita, Mheshimiwa Owen alituletea Hoja kuhusu korosho. Mimea hii miwili hukuzwa sana katika eneo la Pwani. Ni mimea ambayo haina gharama. Ukishapanda mmea wa nazi, huhitaji ufuatiliaji mwingi katika kuulinda mmea huo. Ni mmea ambao unakua wenyewe, na uangaliaji wake ni wa hali ya chini."
}