GET /api/v0.1/hansard/entries/823571/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 823571,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/823571/?format=api",
    "text_counter": 316,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Wundanyi, WDM-K",
    "speaker_title": "Hon. Danson Mwashako",
    "speaker": {
        "id": 13509,
        "legal_name": "Danson Mwashako Mwakuwona",
        "slug": "danson-mwashako-mwakuwona"
    },
    "content": " Asante Mhe. Naibu Spika wa Muda. Nasimama kuunga mkono mapendekezo kufanyia marekebisho ama mageuzi Hoja ambayo imeletwa na Mhe. Owen. Ni Hoja nzuri ambayo sisi viongozi wa Mkoa wa Pwani tunaamini. Si Kilifi peke yake ambako mnazi unakuzwa. Mnazi unakuzwa Pwani nzima. Pili, kiangazi cha mwaka jana na mwaka juzi kiliathiri eneo nzima la Pwani. Kwa hivyo, naunga mkono marekebisho hayo na kusema kwamba Hoja hii imekuja wakati mzuri. Tunajua tuna mimea inayojulikana sehemu nyingi ya Kenya. Ni mimea inayotajika. Inaitwa cash crops kwa Kizungu. Tuko na mimea michache sana kule Pwani. Hatujajulikana sana kwa mambo ya ukulima lakini kwa minazi, mikorosho na mambo kama hayo yanayopatikana kule Pwani, tunatamani Serikali itilie mkazo. Tunapoongea kuhusu zile Ajenda 4 Kuu za Mhe. Uhuru Kenyatta, kilimo kiko ndani. Tunasema Pwani ihesabike moja ya zile sehemu zinachangia kuinua uchumi wa Kenya. Mhe. Owen alitaja kwamba mnazi unawezaleta hata mapato zaidi ya bilioni 13. Ninavyojua, tunawezapandisha hayo mapato tukafika hata bilioni 25 kukuza uchumi huu."
}