GET /api/v0.1/hansard/entries/825323/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 825323,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/825323/?format=api",
    "text_counter": 30,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Wundanyi, WDM- K",
    "speaker_title": "Hon. Danson Mwashako",
    "speaker": {
        "id": 13509,
        "legal_name": "Danson Mwashako Mwakuwona",
        "slug": "danson-mwashako-mwakuwona"
    },
    "content": " Asante sana Naibu Spika wa Muda. Hili swala ambalo limeletwa na Mhe. Jessica Mbalu limenifurahisha kwa sababu limekuja kwa wakati mzuri. Hili swala la wanyama wa pori kuvamia binadamu, mifugo na wanaopakana na Hifadhi ya Tsavo Mashariki na Tsavo Magharibi ni swala nyeti. Juzi nilimsikia Katibu Mkuu wa Wizara husika akisema wanahitaji Ksh15 billion ili waweze kufidia wale wote ambao wana malalamishi kuhusu kuvamiwa na wanyama pori. Swala hili ni nzito sana. Kule Taita Taveta, Wundanyi ninakotoka na kule mwenzangu wa Mwatate anakotoka, umasikini umechangiwa na kuvamiwa na wanyama pori. Hadi leo, ni miaka karibu minne au mitano tangu tuahidiwe kulipwa fidia kwa wale waliovamiwa na wanyama pori na kuawa au mali yao kuharibiwa. Mwezi hata haujaisha, simba wamevamia watu kwa milima. Babu zetu wanatuambia tangu walipozaliwa, hawajawahi kuona simba wakifika kule Wundanyi kwa milima na kule Mwatate Chawia. Leo hii, simba wako kule juu. Hili ni swala ambalo Bunge lazima litilie maanani sana na Kamati ya Mazingira haina budi ila kuleta Ripoti ya kueleweka Bungeni."
}