GET /api/v0.1/hansard/entries/825705/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 825705,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/825705/?format=api",
    "text_counter": 412,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Samburu CWR, KANU",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Maison Leshoomo",
    "speaker": {
        "id": 379,
        "legal_name": "Maison Leshoomo",
        "slug": "maison-leshoomo"
    },
    "content": " Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Naunga mkono Ripoti hii kuhusu IPOA kwa sababu tunaelewa hili ni shirika la kuchunguza maafisa wa polisi wakati wananyanyasa wananchi. Tumepata shida nyingi katika Kaunti ya Samburu mahali ninatoka kwa sababu ya shida ya polisi na wananchi. Tulipopeleka kesi kwa IPOA, ninaamini waliifanya hiyo kesi na kuthibitisha ni nini kilikuwa kimefanyika. Hiyo IPOA iliweka kila kitu wazi. Ninaunga mkono uteuzi wa hawa watu kwa shirika hili kwa sababu tumeona ile kazi linafanya katika Kenya yetu. Hii IPOA haina bajeti ya kufanyia kazi. Naomba kamati husika na Serikali waipe hela kwa sababu mambo mengi yanayofanyika kwa polisi yataisha wakiwa na bajeti. Polisi wanauliwa wakifuatilia mambo ya uhalifu. Sio wananchi peke yao wanauawa. Hata maafisa wa polisi wanapata shida na wanahitaji usaidizi. Hawana magari ya kutosha wala pesa za mafuta. Saa ingine wanashindwa kufanya kazi kwa sababu hawana rasilimali. Kwa kweli, kama wenzangu walivyosema kuhusu polisi, wana shida kubwa sana. Ukiangalia makazi ya Administration Police na General Service Unit, ni duni sana. Ni pahali kama kiwanja ambapo kila mtu anaweza kuingia kupitia kokote. Hawana makao. Familia zao zinaumia. Ndio maana unaona wakati mwingine askari akichukua bunduki na kujiua, ni kwa The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}