GET /api/v0.1/hansard/entries/825872/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 825872,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/825872/?format=api",
    "text_counter": 49,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinya",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Asante sana, Bi Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii. Nilikuwa na hofu, nikidhani kwamba ungenibagua kwa sababu niliona umeanzia na wanadada Maseneta. Nataka kuungana nawe kuwapongeza wenzetu ambao wametoka katika sehemu mbalimbali, hasa Bunge la Kaunti ya Machakos. Naingependa kumpongeza Spika wa Bunge la Kaunti ya Machakos, Bi. Florence, kwa sababu tumekuwa naye katika vikao tofautitofauti. Yeye amemakinika katika kazi yake ya usipika. Nina hakika ya kwamba hata wanadada ambao wako pamoja naye wamemakinika na kubobea katika kazi zao. Ni vizuri sisi kila mara tunapofanya uchaguzi tuwakumbuke wanadada wetu kwa sababu wao hufanya kazi kwa ujuzi wa juu na bila kuegemea upande wowote, kama unavyofanya, Bi. Spika wa Muda. Nimewakaribisha hapa Seneti. Ni maombi yangu watajumuike na sisi ili waweze kujifundisha mengi kutoka Bunge la Seneti. Ni mapenzi yangu kuwa wataenda na mambo ambayo itawasaidia kule mashinani kwa mujibu wa kuwaifidi watu wote katika kaunti yao."
}